VHM

Pages

Wednesday, April 23, 2014

NGUVU NYUMA YA JINA LAKO na Mchungaji Peter Mitimingi.

Picha: BAADHI YA WATU WALIOBADILISHWA MAJINA KATIKA BIBILIA:
THE POWER BEHIND YOUR NAME
Vitabu vinapatikana sasa 5000Tsh

1. Abramu – Ibrahamu – Alibadilishwa na Mungu Mwenyewe
• Tafsiri ya jina Abramu ilikuwa ni MUUMBAJI WA NAFSI (a souls creator; High father), maana ambayo Ilikuwa na uhusiano na mambo ya kishirikina. Ni kama wale wataalam wa kiganga. Alibadilishwa  kwenda Ibrahimu – Baba wa mataifa.
2. SARAI –SARA- Alibadilishwa na Mungu Mwenyewe
• Jina Sarai - lilimaanisha Binti wa kifalme. Tatizo lilikuwa ni binti wa Kifalme, katika ufalme upi. Ndiyo maana Mungu akaamua kufanya badiliko dogo katiaka jina lake.
• Jina Sara - linamaanisha Mwanamke aliye katika ngazi ya juu, mama wa mataifa mengi.
• Mungu alimbadilisha Sarai jina ili kuonesha hatua ya badiliko kutoka katika hatua ya chini kwenda hatua ya juu na kumfanya kuwa mama wa mataifa. (The name-change indicates a step from local to global)
3. Yakobo - Israeli - Alibadilishwa na Mungu mwenyewe.
 
• Jina Yakobo/James – lilimaanisha mtu mdanganyifu, mwenye hila
• Jina Israeli -  linamaanisha taifa la Mungu.
4. Simoni mwana wa Yohana – Petro– Alibadilishwa na Yesu.
• Jina Simoni – lilimaanisha ………………………….
Jina Petro – lilimaanisha jiwe/ mwamba

5. Sauli – Paulo – Alibadilishwa na Yesu
• Sauli ilimaanisha mtu wa maangamizi/kifo (Angalia Sauli wa Agano la Kale alitafuta kumuangamiza Daudi. Aliangamiza watu wengi sana katika utawala wake. Sauli wa Agano Jipya naye alitafuta na kuangamiza wakristo wengi sana mpaka pale alipookolewa.

• Paulo ilimaanisha mtu mdogo aliyejishusha.

6. Daniel  - Belteshaza - Alibadlishwa na mkuu wa matowashi wa mfamle Nebukadreza 
danieli na wenzake walipofika tu uhamishoni, kitu cha kwanza kilikuwa ni kubadilishwa majina yao.
Jina Danieli – lilimaanisha mtumwa w…..
Watu wengine waliobadilishwa majina yao kwenye maandiko utajisomea mwenyewe kwenye kitabu hiki NGUVU NYUMA YA JINA LAKO
BAADHI YA WATU WALIOBADILISHWA MAJINA KATIKA BIBILIA:
THE POWER BEHIND YOUR NAME
Vitabu vinapatikana sasa 5000 Tsh.
 
Kitabu hiki sio cha kukosa. haya ni baadhi tu ya majina na maana zake. Wasiliana na Mchungaji Peter Mitimingi kwa namba 
0713 183939 ili akuelekeza mahali pa kukipata kitabu hiki.
Haya ni baadhi tu ya majina na maana zake kwa ufupi.
 
1. Abramu – Ibrahamu – Alibadilishwa na Mungu Mwenyewe
• Tafsiri ya jina Abramu ilikuwa ni MUUMBAJI WA NAFSI (a souls creator; High father), maana ambayo Ilikuwa na uhusiano na mambo ya kishirikina. Ni kama wale wataalam wa kiganga. Alibadilishwa kwenda Ibrahimu – Baba wa mataifa.
2. SARAI –SARA- Alibadilishwa na Mungu Mwenyewe
• Jina Sarai - lilimaanisha Binti wa kifalme. Tatizo lilikuwa ni binti wa Kifalme, katika ufalme upi. Ndiyo maana Mungu akaamua kufanya badiliko dogo katiaka jina lake.
• Jina Sara - linamaanisha Mwanamke aliye katika ngazi ya juu, mama wa mataifa mengi.
• Mungu alimbadilisha Sarai jina ili kuonesha hatua ya badiliko kutoka katika hatua ya chini kwenda hatua ya juu na kumfanya kuwa mama wa mataifa. (The name-change indicates a step from local to global)
3. Yakobo - Israeli - Alibadilishwa na Mungu mwenyewe.

• Jina Yakobo/James – lilimaanisha mtu mdanganyifu, mwenye hila
• Jina Israeli - linamaanisha taifa la Mungu.
4. Simoni mwana wa Yohana – Petro– Alibadilishwa na Yesu.
• Jina Simoni – lilimaanisha ………………………….
Jina Petro – lilimaanisha jiwe/ mwamba

5. Sauli – Paulo – Alibadilishwa na Yesu
• Sauli ilimaanisha mtu wa maangamizi/kifo (Angalia Sauli wa Agano la Kale alitafuta kumuangamiza Daudi. Aliangamiza watu wengi sana katika utawala wake. Sauli wa Agano Jipya naye alitafuta na kuangamiza wakristo wengi sana mpaka pale alipookolewa.

• Paulo ilimaanisha mtu mdogo aliyejishusha.

6. Daniel - Belteshaza - Alibadlishwa na mkuu wa matowashi wa
mfamle Nebukadreza
danieli na wenzake walipofika tu uhamishoni, kitu cha kwanza kilikuwa ni kubadilishwa majina yao.

Jina Danieli – lilimaanisha mtumwa w…..

Watu wengine waliobadilishwa majina yao kwenye maandiko utajisomea mwenyewe kwenye kitabu hiki NGUVU NYUMA YA JINA LAKO
 

12. Agness Asili ya Kiyunani, na maana yake ni “ safi, takatifu”.
13. Adamson – Asili ya Kiingereza ya zamani, na maana yake ni “mwana wa Adamu”.
14. Aden- Asili ya Kigiliki, na maana yake ni “moto”.
15. Aisha – Asili ya Kiarabu, na maana yake ni “ yu hai na mwenye afya njema”.
16. Aaliya – Asili ya Kiarabu, na maana yake ni “mwenye asili ya kifahari”.
17. Amina – Asili ya Kiarabu, na maana yake ni “aliyemkweli na mwaminifu”.
18. Anisa – Asili ya Kiebrania, na maana yake ni “neema au upendeleo/kibali”.
19. Michael – ni nani aliye kama Mungu.
20. Amani – Asili ya Kiarabu, na maana yake ni “ hamu; matarajio au matakwa”.
21. Samson – Asili ya Kiebrania, na maana yake ni “Jua”.
22. Nicholas – Asili ya Kiyunani, na maana yake ni “watu wa ushindi”.
23. Margaret – Asili ya Kiyunani, na maana yake ni “Lulu mwanamke wa thamani”.
24. Ester – Asili ya Kiajemi, na maana yake ni “Mtu mwororo, jani la mti mwororo,”.
25. Faraja – Asili ya Kiswahili, na maana yake ni “faraja, nafuu au pumziko”.
26. Editha, Edith – Asili ya Kiingereza, na maana yake ni “Mwanamke wa mashindano kwa ajili ya mali”.
27. Jane – Asili ya Kiebrania, na maana yake ni “neema ya Mungu”.
28. Halima – Asili ya Kiarabu, na maana yake ni “mpole, mwenye tabia ya kati.”
29. Linda – Asili ya Kihispania, na maana yake ni “mzuri wa sura”.
30. Flora – Asili ya Kilatini, na maana yake ni “Ua”.
31. Victoria/Victor - Asili ya Kilatini, na maana yake ni “ushindi”.
32. Jessica – Asili ya Kiebrania, na maana yake ni “Anayeona”.


33. Emma – Asili ya Kifaransa na Kijerumani ya zamani, na maana yake ni “yote, ya kiulimwengu

VHM WAVAMIWA NA KUIBIWA WAKIWA NJIANI KUELEKEA KWENYE HUDUMA MKOANI MOROGORO



Kundi la wainjilisti ama makomandoo wa Yesu kutoka huduma ya sauti ya matumaini au The Voice of Hope ministries iliyochini ya mchungaji Peter Mitimingi, wamevamiwa na watu wasiojulikana na kuporwa pesa zote walizokuwa nazo pamoja na vifaa vingine vya kazi wakati kundi hilo likiwa njiani kuelekea Matombo mkoani Morogoro kwaajili ya huduma.

Ambapo kwa mujibu wa mchungaji Mitimingi anasema pesa zilizoporwa pamoja zilikuwa zimehifadhiwa na mweka hazina wa safari hiyo ambaye alijeruhiwa kwa kupasuka kidogo kichwani baada ya kupigwa na chupa ya bia wakati alipojaribu kuleta ubishi wa kutoa pesa kwa watu hao. Kwa mujibu wa mchungaji Mitimingi anasema timu imekwama kuendelea na safari 'tunasubiria neema ye Bwana waendelee na safari ya huko Matombo' amesema mchungaji Mitimingi.

Kuwasiliana na timu ya VHM piga namba hii kwa maswali au kuchangia huduma yao ambayo imefanyika baraka kwa maelfu nchini kwasasa. kwa walionje ya Tanzania anza na +255 713183939 na kwa walio Tanzania piga 0713 183939.

Saturday, April 12, 2014

MADHARA YA WAZAZI NA NDUGU KUMCHAGULIA MTU MUME AU MKE WA KUOLEWA NAYE


 Na Mchungaji Peter Mitimingi


1. Kuchaguliwa mwenza na wazazi. Familia nyingi za Kiafrika huwa zinavunjika kwa sababu hii.

2. Imekuwa ni kawaida hasa kwetu Waafrika kwa sababu ya urafiki wa kifamilia wazazi wa familia hizi mbili wanaweza kuamua na kuchagua wenza wa watoto wao kwa lengo la kuendeleza na kudumisha mahusiano yao kwa kupitia ndoa ya watoto wao.

3. Kuoa au Kuolewa kwa Kuwafurahisha Wanandugu. Kuoa au kuolewa kwa nia ya kutimiza matakwa ya ndugu na wanafamilia wako vilevile ni moja ya sababu zisizo sahihi za mtu kuoa au kuolewa. Ndoa sio ya ukoo ndoa ni ya watu wawili nan i lazima wakubaliane wao wenyewe bila ushawishi wa mtu wa tatu.

4. Kama ilivyo kuoa au kuolewa kunako waumiza wazazi wako, haipaswi mzazi kwa akili zake timamu amlazimishe kwa manufaa yao wenyewe binafsi, kwani itakuwa ni kumuumiza mtoto wake.

5. Hakuna mtoto ambaye kwa kufikiri kwake sawa sawa atafunga ndoa kwa minajili ya kuwaumiza wazazi wake au kuwakera. Ndoa kwa hali hiyo itakuja na changamoto zake na mambo yake, mambo mengine yanaweza kuwa ni magumu sana kuyakabili katika ndoa.

5. Kila mmoja kwa sehemu yake yaani wanaotarajia kuoana au kwa upande wa wazazi, nimuhimu kufuata taratibu zinazohusika ambazo hazitaweza kuumiza upande wowote. Let it be win-win situation. Wazazi washinde na watoto washinde pia.

GWIJI WA UCHAWI KWA MIAKA 80 AKABIDHI MIKOBA YAKE YA UCHAWI MKUTANO WA VHM BAGAMOYO

Mchungaji Peter Mitimingi akinyanyua juu mkoba wa uchawi wa babu  kwa makutano.
Huduma ya sauti ya matumaini ama The Voice of Hope Ministries (VHM) chini ya mkurugenzi wake mchungaji Peter Mitimingi imeendelea kumshinda shetani na kurudisha mateka kwa Yesu safari hii ikiwa katika moja ya vijiji wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Ambapo katika mkutano huo mmoja kati ya magwiji wa uchawi wilayani humo mwenye umri wa miaka 80 amekabidhi mfuko wake wa uchawi na kumpa Kristo maisha yake. Mzee huyo amesema amefanya shughuli za kichawi toka akiwa mtoto mdogo ambapo ameshindwa kukabidhi mtu wa kurithi mikoba hiyo kutokana nayeye kuwa mzee nguvu za mwili zinamuishia hali inayomfanya ashindwe kutimiza majukumu yake inavyotakiwa na kuwakasirisha majini yake ambayo humuangushia kipigo kutokana na ugoigoi wake.
Baada ya kusikia makomandoo wa Yesu VHM wapo kijijini kwake aliamua kwenda kuroga na kukutana na mzinga wa nguvu za Mungu na kujikuta akisalimisha mizigo yake yote ya uchawi kwa watumishi wa VHM ambao bado wanapiga injili kijijini hapo.

Huduma ya VHM imekuwa ikijishughulisha na injili sehemu za vijijini na mijini ambako kuna ugumu wa injili kufikika kwa urahisi hasa kutokana na sifa za kuwepo nguvu za kishirikina ama kutowahi kusikika injili kabisa na watu wamekuwa wakionewa na nguvu za giza. Ili kujua mengi kuhusu huduma hii ama kutaka kuchangia huduma hii ofisi zao zipo Mwenge jijini Dar es salaam karibu na hospitali ya mama Ngoma au wapigie simu ifuatayo 0713 183 939

Muhubiri wa mkutano huo mwinjilisti Lonas Khiwele akiunyanyua juu mkoba wa uchawi wa babu mbele za watu.
Mkoba ukiwekwa sawa kuchomwa moto.
Umati wa watu mkutanoni hapo. 


Wakati wa kumshambulia shetani.
Mfuko wa babu ukichomwa mbele ya umati wa watu.
Kwa Yesu ndiko kwenye usalama wa uhakika, umati ukikubali kumfuata Kristo.

MADHARA YA KUANZISHA MAHUSIANO MAPYA WAKATI BADO UNA MAJERAHA NA VIDONDA VYA ALIYEPITA!

 Na Mchungaji Peter Mitimingi

Kabla ya kupanda mbegu mpya ya upendo kwa mtu, ni lazima mtu achukue muda wa kutosha kushughulikia na madondo na majeraha yaliyotokana na mahusiano ya nyuma na mtu aliyekuumiza au kukujurehi. 

Watu wengi hufanya makosa wakidhani kuwa njia pekee ya kupona dhidi ya majeraha ya maumivu yaliyopita ni kutafuta mtu mwingine katika mahusiano atakaye chukua nafasi ya yule aliyemsababishia kuumia. 

Hilo ni kosa ambalo badala ya kuleta faraja na upendo anaoutafuta atajikuta anajiumiza mwenyewe na kumuumiza mwenzake na pia yeye kuumizwa zaidi ya mara ya kwanza. 


Unashauriwa kabla hujaanzisha mahusinao na mtu mwingine ni lazima uwe na muda wa kutosha kupona madonda kwanza ndipo utakuwa na ndoa yenye baraka na amani.


KANUNI 10 ZA VIJANA KUJIANDAA KABLA YA NDOA!



Na Mchungaji Peter Mitimingi

1. Jifanyie Maboresho wewe Mwenyewe yaani Imrove yourself.

2. Anza kujifunza sifa juu ya mume mzuri yukoje na Mke mzuri yukoje.


3. Tafuta kujua Baba mzuri anakuwaje au mama mzuri anakuwaje.
4. Jifunze kuwa mkomavu sio kudeka deka kwa vitu vidogo unataka mpaka wazazi wakufanyie. Mfano kuna baadhi ya vijana ni "MIJEBA" lakini bado wanaomba pesa za kunyolea ndevu kutoka kwa wazazi wao halafu unataka kuwa mume..


5. Jitahidi kuhudhuria mafunzo mbalimbali juu ya mambo ya kabla ya ndoa "pre-marital trainings, seminars.


6. Soma vitabu mbalimbali vya mambo yahusuyo namna ya kuingia kwenye ndoa.


7. Sikiliza vipindi vya vyombo vya habari vinavyofundisha mambo yahusuyo kuingia kwenye ndoa.


8. Jifunze mambo Mema na uyafuate na usitafute mifano ya walioshindwa katika ndoa zao kama nguzo ya kuegemea.


9. Rudisha Tabia njema za zamani ulizoziacha.


10. Epuka misimamo migumu na isiyo ya msingi ya kimila au kimakabila zingatia nyakati na utakatifu.

JIFUNZE KITU KUHUSU HUYU OMBA OMBA WA BARABARANI AMBAYE NI MFADHILI WA VHM!


Msimulizi ni Mchungaji Peter Mitimingi wa VHM


Huyu dadani mlemavu wa miguu. ni moja ya wadada ambao wananibariki sana mimi binafsi na kuubariki moyo wa Mungu.


Nilikutananaye mara ya kwanza kwenye makutano ya mataa "traffic light" akiwa kwenye wheelchair yake akiomba msaada wanaosimamisha magari.


Alinisikia nikiongea radioni kwahabari ya kuchangia kupeleka injili vijijini akanipigia simu na kunielekeza kijiwe anachoombea pesa na akasema amejibana kwa muda mrefu ana anataka kuchangia huduma ya VHM vijijini nikachukue sadaka yake hapo barabarani.


 Tulipokwenda dada huyu alitoa Tsh 21,000 alizokusanya kwa muda mrefu. Tulimuombea Baraka baada ya hapo akasema watu walianza kumpa pesa sio tu vicoin alianza kurushiwa elfu 1, elfu, 2, elfu 5 hadi elfu kumi.

Baada ya muda dada huyo aliniita tena kwenda kuchukua sadaka yake na safari hii dada huyo alitoa elfu 50. Tukamuombea tena baada ya muda alileta doti 6 za vitenge vya wax Piece tatu tatu kwajili ya wake za wachungaji vijijini. 


Tukamuombea tena. Baada ya muda akaleta Mashuka ya 6x6 na foronya zake kwajili ya wachungaji wa vijijini tukamuombea tena.
Juzi jumamosi miaka miwili baadaye nikashangaa kumuona nje ya ukumbi wa Msimbazi center nilipokuwa nimealikwa kufundisha wanandoa akiwa sio omba omba tena wa barabarani bali akiwa anamiliki biashara yake hiyo ya vitu mbalimbali kama anavyonikana katika picha.
                      CHANGAMOTO:

kuna watu wana miguu, mikono viungo vyote, wana kazi nzuri au biashara nzuri lakini kwa swala la kumtolea Mungu wamekuwa mbinde sana na visingizio na sabubu nyingi sana SIJUI UTAJIBU NINI KWA MUNGU SIKU HIYO AKIMSIMAMISHA DADA HUYU NA WEWE KUTOA HESABU YA ULICHOFANYA DUNIANI KWAJILI YA MUNGU
tafakari.

KANUNI 10 ZA MBOLEA ZA MANENO YA KUTIA MOYO KWA WANANDOA


Na mchungaji Peter Mitimingi

1. Wanawake wengi wananjaa ya kusikia maneno mazuri kutoka kwa waume zao. Lakini wanaume ni wagumu sana kusifia wake zao wengi hupenda kusifia wanawake wengine kule nje lakini sio mke wake. Jambo hilo huwakwaza sana wanawake.

2. Usiwe mtu wa kukatisha tamaa katika kila jambo kwa kutoa kauli mbaya na ngumu kwa mwenzi wako. Unamkatisha tamaa mkeo kwamba hawezi kitu au unamkatisha tamaa mumeo kwamba hanalolote ni sawa na mvaa suruali tu. Huko siko kujenge ndoa imara.

3. Hata kama jambo ni gumu kiasi gani usionyeshe hali ya kukatisha tamaa na kumvunja moyo. Tumia mbinu kuinua kiwango cha moyo cha mwenzi wako na kubadilisha hali madhaifu yake kuwa mafanikio. Mtie moyo mwezi wako aendelee mbele na sio kukata tamaa na kumrudisha nyuma.

4. Kabla hujatamka neno hakikisha ni maneno yaliyopata kibali kabla ya kutamkwa. Jiwekee chujio mdomoni kabla ya kutamka. Chuja maneno yote yaliyobeba sumu inayojeruhi moyo wa mwenzi wako kabla hujatamka. Midomo yako iteme asali kwa mwenzi wako sio iteme sumu.

5. Mwenzi wako ni rafiki yako, rafiki mara zote huambiwa maneno mazuri. Usitumie maneno ya ukali kwa mwezi wako mpaka akawa na hofu kukushirikisha kitu kwa kuhofia majibu makali atakayo yapokea kutoka kwako.

6. Usitumie maneno ya kashfa kwa mwenzi wako. Usitumie maneno ya kumdharilisha hata kama kweli kakosea. Hatakama unataka kueleza tatizo la mwenzi wako tumia maneno mazuri kumueleza na kwa wakati muafaka.

7. Mwenzi wako akifanya jambo zuri jitahidi kumpongeza, nakuonyesha kwamba kweli kafanya jambo zuri. Usichukulie kwamba ni jambo zuri na likaishia moyoni mwako. Usijikaushe liseme wazi. (speak it out) Akipika vizuri mpongeze, akivaa vizuri mpongeze kama ni mume akifanya vizuri kazini mpongeze.

8. Mpongeze mwenzi wako mbele za watu wengine, watoto wenu, wazazi wake marafiki zako au marafiki zake hiyo inajenga ujasiri mkubwa na kujiamini sana kwa mwanandoa anayepongezwa mbela za watu wengine n.k

9. Mpongeze mwenzi wako mbele za watu wanao mchukia au kumdharau sana. (Maadui zake). Hiyo itamjengea kujithamini na kupata uhakika wa kujiona kuwa yeye tayari ni mshindi pia itamuondolea hofu na kujidharau.

10. Maneno yanaumba. Ukimtamkia mwenzi wako maneno mabaya basi ujue hayo mabaya yatamfuata. Ukimtamkia mwenzi wako maneo mazuri basi ujue mambo mazuri yatamfuata.

KANUNI 12 YA KUIMARISHA MUDA WA THAMANI NA MWENZI WAKO


Na Mchungaji na Mwalimu Peter Mitimingi, Mkurugenzi wa Huduma ya The Voice of Hope Ministry(VHM)

1. Hakikisha kwamba unarudi nyumbani mapema katika muda mzuri baada ya kazi zako za siku.

2. Ukifika nyumbani usifikie kwenye Tv, magazeti, Kompyuta au mambo yako binafsi.

3. Jambo la kwaza liwe kukaa na mwenzi wako na kupata taarifa kwa kifupi ya mambo yaliyojili wakati ulipokuwa haupo.

4. Usipeleke cheo chako nyumbani au kazi zako za ofisi au biashara zako nyumbani kwa mkeo au watoto.

5. Mtazame mwenzi wako wakati mnapozungumza usiangalie pembeni au kwenye simu au Tv au kwingineko.

6. Usimsikilize wakati huo huo unafanya jambo linguine labda unapika au unafua au unachambua mchele au unasoma magazeti nk.

7. Sikiliza kwa hisia na uonyeshe kwamba hisia zako zipo pamoja naye. UUnge mkono kwa kuitikia, au kuonyesha mshangao, au kwa kucheka nk.

8. Usiwe mwingi wa kuzungumza bali utumie muda mwingi kisikiliza (hasa kwa wanaume). Zingatia kanuni ya kusikiliza. Wanaume huongea maneno 6,000 kwa siku na wanawake huongea maneno 24,000 kwa siku.

9. Tengenezeni utaratibu wa kutoka nje pamoja (Outing) sehemu za tofauti na zile mlizo zizoea. Mtoe mkeo au mumeo na watoto outing mara moja moja.

10. Mnapotembea muongozane pamoja. Msiachane au mmoja natangulia na mwingine anafuatia nyuma hiyo inaleta picha mbaya kusomeka kwa watu na huwa ni dalili za kuanza kutengana kwa siku za usoni.

11. Mle chakula kwa pamoja sio kila mtu kula kwa wakati wake. Kuna nguvu sana kwa wanandoa kula chakula pamoja.

12. Muwe na wakati wa maongezi na ibada pamoja kama mke na mume na watoto pia.

TAFSIRI YA NAMBA 4 KIBIBLIA



Na Mchungaji na Mwalimu Peter Mitimingi, Mkurugenzi wa Huduma ya The Voice of Hope Ministry(VHM)

TAFSIRI YA NAMBA 4 KIBIBLIA
Tumeuanza mwezi wa 4. 2014


Namba NNE ni namba ya uumbaji.


1. Katika siku ya NNE Mungu alikamisha kuumba vitu.

2. Kuna pande kuu NNE zinazokamilisha dunia, (Kaskazini, Kusini, Mashariki na Magharibi (Isa 11:12).

3. Katika Hekalu la Ezekiel kulikuwa na meza za sadaka NNE upande mmoja na NNE upande mwingine.

4. Siku imegawanyika katika sehemu NNE. (Asubuhi, Mchana, Jioni na Usiku).

5. Katika amri kumi, amri NNE zinahusisha zaidi juu ya dunia.

6. Injili NNE zinawakilisha maisha ya Yesu hapa duniani.

7. Wanawake wa-NNE wametajwa katika mlolongo wa kuzaliwa kwa Yesu. (Thamar, Rahabu, Ruth na Mke aliyekuwa wa Huria).

8. Kuna vijana wa-NNE wa-Kiebrania waliotajwa katika kitabu cha Daniel.

9. Kuna wafalme wa-NNE waliotajwa katika kitabu cha Dniel. (Nebukadineza na Belshashaza wa wafalme wa Babeli, wengine ni Dairo na Silas wa Uajemi).

10. Ezekieli inazungumza juu ya Hukumu NNE juu ya Dunia.

11. Vizazi vi NNE vilionwa na Ayubu kabla ya kufa kwake (Job 42:166)

12. Kambi ya waisrael iligawanyika katika sehemu kuu nne Hesabu 2:1-34

13. Baada ya Yesu Kutungikwa msalabani askari wa kirumi waligawanya vazi la Yesu vipande vine kila kipande kwajili ya kila mmoja wao. Yoh. 19:23

14. Kuna vipindi muhimu vinavyo ongoza majira katika dunia.(1. Fall 2. Winter 3. Spring 4. Summer)

15. Siku imegawanyika katika vipindi vine. (1. Asubuhi 2. Mchana 3. Jioni 4. Usiku)

16. Yesu alitoa mfano wa aina nne za Udongo. Mathayo 13.

Namba NNE ni namba ya uumbaji.
Ninamuomba Mungu katika mwezi huu wa 4 Aumbe jambi jipya katika mwezi huu uwe mwezi ambao utauma mafanikio na baraka katika maisha yako.

MADHARA 10 YA MOYO ULIOJERUHIWA


 Na Mchungaji Peter Mitimingi

1. Moyo uliojeruhiwa huwafanya watu waishi katika hali ya kuumizwa.

2. Moyo uliojeruhiwa huwa na tabia za kuharibu na bila kujali.


3. Moyo uliojeruhiwa humfanya mtu awe hana hisa za utu.


4. Moyo uliojeruhiwa humfanya mtu kuwa na hasira za ghafla wakati mwingine zisizo na msingi.


5. Moyo uliojeruhiwa humfanya mtu kwa na tabia ya kujitenga.


6. Moyo uliojeruhiwa huwa na hali ya kukata tamaa kwa hali ya juu


7. Moyo uliojeruhiwa huwa tayari kwa kupigana na kwa mapambano.


8. Moyo uliojeruhiwa humfanya mtu kuwa na ubinafsi uliozidi kiwango.


9. Moyo uliojeruhiwa humfanya mtu kuwa na woga usio na mipaka.


10. Moyo uliojeruhiwa humfanya mtu kujiona kuwa huwa hukosei.

YALIYOJIRI KATIKA KONGAMANO LA VIJANA CCC UPANGA.



Picha: MOJA YA TULIYOJIFUNZA NI UTANDAWAZI NA MAADILI MEMA KWA VIJANA
Mchungaji   Mitimingi akifundisha  jana.
Jana jumatatu tarehe 07 April 2014 kulikuwa na kongamano kubwa la vijana lililofanyika katika ukumbi wa kanisa la City Christian Center(CCC Upanga). Mwalimu katika kongamano hilo alikuwa ni Mchungaji Peter Mitimingi. 

Maelfu wa vijana walihudhuria na hakika BWANA YESU alitwaa utukufu maana hata waliompokea kuwa BWANA na MWOKOZI wa maisha yao walikuwa ni wengi. 

Mchungaji  Peter Mitimingi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Huduma ya The Voice of Hope Ministry(VHM) alifundisha na katika Topic zilizogusiwa ni pamoja na

• AINA 10 ZA ZINAA
• MADHARA YA VIJANA KUJICHUA
• MADHARA YA KUANGALIA PICHA ZA NGOZO
• SABABU 10 ZA VIJANA KUFANYA TENDO LA NDOA KABLA
• UTHAMANI NA FAIDA ZA UBIKIRA KWA VIJANA
• MADHARA YA KUFANYA TENDO LA NDOA KABLA YA NDOA
• NJIA ZA KUDHIBITI TAMAA ZA MWILI
• ATHARI ZA MIGUSANO YA MWILI WAVULANA NA WASICHANA
• MTAZAMO WA MUNGU JUU YA MAISHA YA KIJANA


Haya ni baadhi ya matukio katika picha.MUNGU akubariki.
Baba Askofu Dr. Ranwel Mwanisongole Ndiye Aliyekuwa Mgeni Rasmi katika Kongamano la Vijana
Waandishi wa Habari Pia Hawakuwa nyuma kuchukua habari kulikoni vijana kumiminika hapa leo!
Baadhi ya Vijana wakiwa kwenye Ukumbi wa Nje Baada ya Ukumbi wa Ndni kufurika Vijana walikaa nje na kufuatilia somo wakiwa nje
 Vijana wakifuatilia fundisho kupitia screen iliyowekwa kwa nje baada ya ukumbi wa ndani kujaa
BAADHI YA VIJANA WALIOPITA MBELE KUSALIMISHA MAISHA YAO KWA BWANA YESU KATIKA KONGAMANO LA VIJANA UPANGA CCC
MAKOMANDOO WA VHM HAWAKUWA MBALI KATIKA KUWAHUDUMIA VIJANA KWENYE KONGAMANO
VIJANA WALIOMPOKEA BWANA YESU WAKIJAZA FOMU MAALUM BAADA YA KUOMBEWA SALA YA TOBA KATIKA KONGAMANO LA VIJANA UPANGA CCC
VIJANA WALIFURIKA UKUMBI WA KANISA LA CCC UPANGA WAKIWA NA KIU NA SHAUKU YA KUPOKEA MAFUNDISHO